Imezoeleka katika mpira wa miguu, (mchezo unaoaminika kuwa na mashabiki wengi duniani) kuwa mchezaji anapovunja sheria mojawapo kati ya 17 za mchezo huo huadhibiwa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mchezaji SALIH DURSUN anayechezea klabu ya Trabzonspor inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki alionyesha kali ya mwaka baada ya kumuonyesha KADI NYEKUNDU Mwamuzi DENIZ BITNEL aliyekuwa akichezesha mchezo huo..
Trabzonspor ilifungwa magoli 2-1 na Galatasaray katika mchezo ambao mchezaji huo aliyejizolea umaarufu toka kwa mashabiki wake, alikuwa mchezaji wa nne kuonyeshwa kadi nyekundu huku mwamuzi wa mchezo huo akisemwa kwa maamuzi mabovu.
Timu hiyo imedai kuwa iko katika maandalizi ya kulijengea mnara tukio hilo.