Thursday, May 19, 2016

AJALI ZA NDEGE : NDEGE NYINGINE YAPOTEA

Ndege ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir
iliyokua ikitokea Jumatano usiku katika uwanja
wa mji wa Paris ikielekea Cairo, nchini Msri
imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada,
ikiwa na abiria 56 na wafanyakazi 10, shirika la
ndege la Misri limetangaza mapema Alhamisi hii
asubuhi.
Ndege hii imetoweka ghafla kutoka kwenye
mitambo ya rada wakati ambapo ilikua ikipaa
angani katika eneo la bahari ya Mediterranean.
Ndege hii ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir
iliyokua ikitokea katika uwanja wa ndege wa
Charles de Gaulle mjini Paris ikielekea Cairo,
nchini Msri, imetoweka Alhamisi hii asubuhi na
mapema, ikiwa naabiria 56 na wafanyakazi 10.
Ngege hii yenye chapa MS804 ilikua ikipaa
katika eneo la bahari ya Mediterranean katika
anga baa ya kuingia kilomita 16 katika anga ya
Misri.
Shirika la ndege la EgyptAir limeonya mamlaka
husika na kusema kuwa timu za waokoaji
zimeanza shughuli ya kutafuta ndege hiyo, na
kubainisha kuwa "ndege imetoweka kwa rada"
baada ya kuingia katika anga ya Misri na
kusafiri kilomita 16.
Abiria waliokuwemo ndani ya ndege A320
Awali, shirika la ndege la EgyptAir ilitangaza
kuwa kulikuwa na abiria 59 na wafanyakazi 10.
Kwenye akaunti yake Twitter, EgyptAir
hatimaye imesahihisha takwimu zake, na
kusema kwamba kulikuwa na abiria 56, ikiwa ni
pamoja na watoto 3 - na wawili wachanga.
Wafanyakazi 7 walikuemo ndani ya ndege hiyo
pamoja na maafisa 3 wa usalama. Kwa jumla,
watu 66 walikuemo ndani ya ndege hiyo.

Share: