Tsai Ing-wen kutoka chama cha Democratic Progressive Party (DPP) ameapishwa kuiongoza nchi ya TAIWAN
Tsai In-wen, ambaye chama chake kinataka uhuru kutoka Uchina, alishinda na idadi kubwa ya kura katika uchaguzi uliofanyika mapema January.
Ushindi wake umepunguza uhusiano wa taifa hilo na utawala wa Beijing.
China inadai kuwa Taiwan ni Mamlaka yake na kutokana na hatua ya sasa ya Taiwan na hata wakati wa Uchaguzi,China imeonekana kutokubalianana Taiwan.
Tsai anakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kushuka kwa mapato yatokanayo na usafirishaji wa bidhaa nje.