Friday, May 20, 2016

TAARIFA KUHUSU NDEGE YA EGYPTAIR ILIYOPOTEA

Jeshi la Misri limepata mabaki
ya ndege hiyo kilomita 290
kaskazini ya Cairo. Baadhi ya
mizigo ya abiria waliokuwemo
ndani ya ndege hiyo pia
imepatikana. Kinachotafutwa
sasa ni kisanduku cha
mawasiliano au "black box"

Juhudi za kutafuta kisanduku
kinachorekodi mawasiliano au
Black box cha ndege hiyo
inaendelea. Ndege hiyo ya
Misri ilianguka usiku wa
kuamkia Alhamisi ikiwa na
abiria 66 miongoni mwao
wahudumu wa ndege hiyo.
Shughuli ya kutafuta mabaki
yake ilianza jana na sasa
imezaa matunda baada ya
kupatikana kwa mabaki ya
ndege hiyo kilomita 290 kutoka
Cairo pamoja na baadhi ya
mizigo ya abiria waliokuwemo
ndani yake pia imepatikana.
Waziri wa safari za anga nchini
Misri amesema uwezekano
kuwa ndege hiyo
ilishambuliwa kigaidi angani ni
mkubwa kuliko hitilafu za
mitambo kusababisha
kutoweka kwake.
Waziri mkuu wa Misri Sherif
Ismail alipoulizwa uwezekano
wa njama ya kigaidi katika
mkasa huo amejibu kuwa
hawapuuzilii sababu yoyote
inayoweza kukisiwa
kusababisha ndege hiyo
kuanguka.
Sababu ya kutoweka ni nini?
Vikosi vya usalama vya Misri
vikishirikiana na vikosi kutoka
Ugiriki vinaendeleza shughuli
za kutafuta mabaki zaidi katika
bahari ya Mediterania.
Waziri wa ulinzi nchini Ugiriki
Panos Kammenos amesema
ndege hiyo aina ya Airbus
ilifanya mizunguko miwili ya
ghafla angani na kushuka
ghafla kutoka futi 37,000 hadi
futi 15,000 angani, kisha
ikatoweka kutoka kwenye
mtambo wao wa rada.

Awali rais wa Ufaransa
Francois Hollande alikariri
kuwa uchunguzi kamili
unahitajika kubaini mkasa huo
umesababishwa na nini.
Maafisa nchini Misri
wamesema kuwa ndege ya
taifa hilo iliyokuwa ikisafiri
kutoka Paris Ufaransa
kuelekea Cairo imetoweka na
huenda imeanguka katika
bahari ya Mediterrania. Ndege
hiyo ya shirika la EgyptAir
ilikuwa na jumla ya watu 66
miongoni mwao wahudumu
wa ndege hiyo. Shughuli za
kutafuta mabaki ya ndege na
manusura imeanzishwa.
Ndege hiyo ilitoweka na
kutoonekana tena kwenye
mtambo wa rada dakika 45
kabla ya muda kamili ambao
ilitarajiwa kutua katika uwanja
wa ndege wa Cairo. Maafisa
nchini Misri wanasema ndege
hiyo ilianguka mwendo wa saa
nane usiku majira ya Misri,
jumla ya saa tatu na nusu
tangu kupaa kutoka uwanja wa
ndege wa Charles de Gaulle
mjini Paris. Hii ni muda mfupi
baada ya ndege hiyo kutoweka
na kutoonekana tena kwenye
mtambo wa rada maili kumi
ndani ya anga ya Misri.
Jamaa za abiria waliokuwemo
ndani ya ndege wamekuwa
katika uwanja wa ndege wa
Cairo wakisubiri habari zaidi
kuhusu wapendwa wao.
Miongoni mwa waliokuwemo
ndani ya ndege hiyo aina ya
MS804 ni raia 30 wa Misri,
wafaransa 15, wairaqi 2, watoto
wawili na mmoja mdogo,
Uingereza, Kuwait, Ubelgiji,
Saudi Arabia, Sudan, Chad,
Ureno, Algeria na Canada
wakiwa na raia mmoja mmoja.

Habari kwa hisani ya mhariri
Deutsche.de

Share: