Friday, May 20, 2016

JIPYA KUHUSU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI-EAC

Alama za Jumuia ya Afrika Mashariki ikiwemo
Bendera na wimbo maalumu zitaanza kutumika
katika taasisi na idara za serikali za nchi
wanachama.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa mkataba wa
uanzishwaji wake.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
serikalini wa Wizara ya mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania,
Mindi Kasiga, kuanzia ngazi ya chini kwenye
serikali za mitaa ambako bendera ya taifa inapepea
ni lazima ya jumuia hiyo iwepo.
Aidha amesema pia kwenye shughuli rasmi za
serikali, wimbo wa taifa unapoimbwa ni lazima pia
wa Afrika mashariki uimbwe pia.
Jumuia ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi
ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya Burundi,
Rwanda, Sudan Kusini.

Share: