Saturday, May 28, 2016

TOENI HOFU KWA MV. KIGAMBONI

Kivuko
cha
MV
Magogoni
kimesitishwa
kutoa huduma kwa muda wa
siku mbili kufuatia kuharibika
kwa mlango wa upande mmoja
wa kivuko hicho.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar
es salaam na Kaimu Mtendaji
wa TEMESA Eng.Marcellin
Magesa kupitia taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya
habari.
Aidha taarifa hiyo imesema
kutakuwa na kivuko kimoja cha
MV Kigamboni kitakachokuwa
kikitoa huduma kwa waenda kwa miguu,baiskeli
pikipiki na mikokoteni.
“Wakati matengenezo haya yanaendelea kivuko cha
Mv Kigamboni pekee ndicho kitakachoendelea kutoa
huduma kwa waenda kwa miguu,baiskeli,pikipiki na
mikokoteni”.alisema Kaimu Mtendaji Mkuu
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa wenye
magari wote watatakiwa kutumia njia ya Kongowe
mpaka kivuko kitakapopona.
Amefafanua sababu ya wenye magari kuombwa
kutumia njia ya kongowe ni pamoja na kivuko
kutokuwa na uwezo wakusafirisha watu wengi
pamoja na mizigo mikubwa.
Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) limetoa boti zake mbili kwa ajili ya kusaidia
kuvusha watu katika kivuko hicho cha Kigamboni.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano,imesema boti hizo za Kamandi ya
wanamaji,Kigamboni zitafanya kazi mpaka kivuko
cha MV Magogoni kitakapopona.
“Kutoa huduma au msaada kwa wananchi ni
sehemu ya majukumu ya JWTZ ya msingi ya
kusaidia wananchi na mamlaka za kiraia pale
yanapotokea matatizo au majanga yanayohusu jamii
moja kwa moja.”Ilisema taarifa hiyo.
Boti hizo mbili za JWTZ zimekuwa zikivusha abiria
tangu Januari Mosi 2011 kati ya Kigamboni na
Magogoni ambapo zitaendelea kutoa huduma hiyo
hadi pantone ya “ MV Magogoni” kitakapokuwa
tayari kwa kazi hiyo.

Share: