Saturday, May 21, 2016

KISWAHILI : UTAMU WAKE

YALIYOMO
MAANA YA FASIH NA
UCHAMBUZI WA VIPERA
MAANA NA METHALI
ZILIZOKUSANYWA
FILAMU NI SEHEMU YA FASIHI
YA KISWAHILI
MAANA YA FASIHI NA
UCHAMBUZI WA VIPERA VYAKE
Williady, (2015) Fasihi ni tawi moja wapo la sanaa
linalotumia lugha katika kuwasilisha ujumbe wa
mdomo au wa maandishi.
Wamitila (2004) Fasihi ni sanaa inayotumia luha na
ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na
maisha yake na huathri, hugusa au huacha athari
fulanina hupatikana katika umbo ambalo
linatambuliwa na jamii Fulani.
Kwakuwa fasihi ni aina ya sanaa, ni vyema
mwanafunzi akajua pia maana ya sanaa.
MAANA YA
SANAA
(Williady: 2015) Sanaa ni ujuzi au ufundi wenye
kuleta manufaa kwa uma.
UMBO LA
SANAA
Tunaposema umbo la sanaa tunamaanisha matawi
yanayojenga sanaa. Matawi hayo nipamoja na;
Fasihi, maonyesho, ususi, uhunzi, ufumaji, utarizi,
uchongaji, ufinyanzi, uchoraji na muziki.
AINA/ KUMBO/ TANZU ZA
FASIHI
Katika kumbo ya fasihi na taaluma zake kuna aina
kuu mbili za fasihi, ambazo ni;
Fasihi Simulizi
Fasihi Andishi
TOFAUTI KATI YA FASIHI
SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI
Namna ya uwasilishaji wake. Fasihi simulizi
huwasilishwa kwa njia yam domo wakati fasihi
andishi uwasilishwa kwa njia ya maandishi.
Mabadiliko. Fasihi simulizi huweza kupokea
mabadiliko ya papo kwa papo wakati fasihi andishi
hurekebishwa baada ya toleo jipya.
Utendaji wake kwa hadhira na fanani. Hadhira na
fanani katika fasihi simulizi huwa ni yakiutendaji,
wasikilizaji wanaweza kuchangia mawazo kwa
kutoa maoni, kuuliza maswali au kushadadia
masimulizi ya fanani. Fasihi andishi hadhira
hawawezi kuchangia lolote.
Ukongwe. Fasihi simulizi niyazamani zaidi, ilianza
wakati mwanadamu alipoanza kutumia mdomo
katika mawasiliano. Fasihi andishi ilianza pindi
maandishi yalipobuniwa.
Vidato na elimu. Fasihi simulizi haiitaji mtu ajue
kusoma ama kuandika, inamuhitaji mtu mwenye
uwezo wa kuzungumza. Fasihi andishi inamhitaji
mtu anayejua kuandika na kusoma.
Umiliki. Fasihi simulizi inamilikiwa na jamii nzima
wakati fasihi andishi humilikiwa na mwandishi
aliyeandika na kupiga chapa kazi hiyo.
Idadi ya tanzu. Fasihi simulizi inatanzu nyingi
zaidi kuliko fasihi andishi.
Kuhifadhi. Hapo kale fasihi simulizi ilihifadhiwa
kichwani, kwa sasa fasihi simulizi yaweza
kuhifadhiwa katika vinasa sauti, kaseti na santuri.
Fasihi andishi yenyewe huifadhi wake ni kwa njia
ya maandishi.
Mwingiliano wa tanzu kwa kiasi. Fasihi simulizi
huweza kuingiliwa kwa kiasi kikubwa na tanzu
nzingine kama vile methali, vitendawili, nyimbo na
nahau wakati fasihi andishi huweza kuingiliwa na
tanzu nyingine kwa kiasi kidogo.
UFAFANUZI WA AINA
ZA FASIHI
1.Fasihi
simulizi
Fasihi simulizi ni aina ya fasihi inayotumia mdomo
na utendaji wa viungo vya mwili katika kuwasilisha
maudhui ya fanani kwa hadhira iliyokusudiwa.
TANZU ZA FASIHI
SIMULIZI
Hadithi, uigizaji, ushairi na
semi
VIPERA VYA HADIDHI
Ngano, vigano, hekaya, soga, tarihi, visa, visasili,
shajara, istiala, michapo na mbazi
VIPERA VYA
UIGIZAJI
Miviga, michezo ya jukwaani, majigambo, utani,
vichekesho, ngonjera, mgomezi na
mazungumzo
VIPERA VYA
USHAIRI
Nyimbo, maghani, ngonjera, mashairi, tenzi na tendi
AINA ZA NYIMBO
Bembezi, nyimbo za mapenzi, nyiso, nyimbo za jadi,
nyimbo za harusi, nyimbo za watoto
nyimbo za sifa, nyimbo za kampeni, nyimbo za
maombolezo na nyimbo za chombezi.
VIPERA VYA SEMI
Methali, misimu, lakabu, nahau, vitendawili. utani,
misimu, mafumbo, masaguo, mizungu na
misemo
MAJUKUMU / DHIMA ZA FASIHI
SIMULIZI KATIKA JAMII
elimisha, kuburudisha, kusisimua, ukombozi, kutoa
mwongozo kwa jamii, kutunza amali
za jamii (historia na utamaduni), kujuza na
kuunganisha vizazi nz vizazi, kufundisha,
kudumisha uhusiano, kudumisha ushirikiano na
kukuza stadi za lugha
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
KATIKA USIMULIZI WA HADITHI
Ili msimuliaji aweze kutongoa au kusimulia hadithi
kwa usahihi inampasa awe na weledi wa kutosha
juu ya mbinu za kusimulia hadithi. Mbinu hozo ni
hizi;
A)
Dhima na maudhui
Msimuliaji wa hadithi anapaswa kujua lengo kuu
(dhima) la hadithi yake. Vilevile msimuliaji
anapaswa kujua maudhui ambayo ni jumla ya
mambo yote yanayopelekea hadithi kutiririka vizuri
kwenye mkondo wake.
B)
Msuko
Msuko wa matukio kwa jina jingine unafahamika
kama muundo. Kipengele hiki cha muundo
kinahusu mpangilio wa hadithi kuanzia mwanzo
mpaka mwisho.
C)
Kusisimua
Kusisimua ni mbinu inayovuta umakini kwa watu.
Msimuliaji anaweza kutumia mbinu kadhaa
zitakazo msisimusha msomaji, mbinu kama vile
taharuki, miguno na kelele za kutisha.
D)
Urudufishaji
Huu ni urudiaji rudiaji katika fasihi simulizi. Mara
nyingi msimuliaji anashauriwa kurudia rudia
maneno, falsafa, nahau au vitendawili vilivyobeba
lengo kuu la hadithi yake.
E)
Chombezo
Chombezo ni kipengele kidogo kinacho elezwa na
mtambaji wa hadithi chenye lengo la kupunguza
ukakasi ama ukalia ama vitisho vilivyotokana na
maudhui ya hadithi Fulani.
F)
Nyimbo
Nyimbo zina kazi nyingi katika masimulizi ya
hadithi. Moja wapo ya matumizi hayo ni kama vile
kuondoa uchovu kwa wasikilizaji, kuvuta usikivu,
kuwakaririsha hadhira falsafa au lengo kuu la
hadithi hiyo.
MAMBO MENGINE
a) Utulivu kwa hadhira
b) Ujenzi wa wahusika
c) Matumizi ya
tamathali za semi
d) Ujenzi wa taswira
2. FASIHI
ANDISHI
Williady (2015) fasihi andishi ni aina ya fasihi
inayowasilishwa kwa ustadi wa maandishi yenye
kuleta maana.
Wamitila (2004) fasihi andishi ni sanaa
inayowasilishwa kwetu kwa maandishi.
TANZU ZA FASIHI
ANDISHI
RIWAYA (NATHARI)
USHAIRI (NUDHUMU)
TAMTHILIYA (SANAA ZA
MAONYESHO)
FANI NA MAUDHUI
KATIKA FASIHI
Fani na maudhui katika fasihi ndio maumbo mawili
makuu yanayobeba sanaa hii.
FANI
Fani ni ufundi unaotumiwa na msanii katika
kufikisha ujumbe uliokusudiwa, fani sio ujumbe bali
ni mfano wa kipaza sauti kinachotumika kufikisha
ujumbe.
VIPENGELE VYA
FANI
Fani inavipengele vingi, kila kipengele kina husika
kipekee kwa kutofautiana na kipengele kingine.
Vipengele vya fani
ni pamoja na;
a) Muundo
Kipengele hiki hutumiwa kueleza mpangilio wa kazi
ya kifasihi. Kwa ufupi kwenye kipengele cha
muundo tunaangalia umbo la kazi ya fasihi, mfano
kazi yaweza kugawanywa katika sura mbalimbali,
sura hizi ndizo ujenga muundo.
b) Mtindo
Williady (2015) mtindo ni mbinu za kipekee
zinazomtofautisha msanii mmoja na mwingine.
Mfano katika fasihi simulizi kipengele cha nyimbo
hadhira inaweza kusikia wimbo kwa mara ya
kwanza na kutambua wimbo huo umeimbwa na
nani bila ya kuambiwa na mtangazaji, hii huweza
kutokea pindi mwimbaji mashuhuri anayetumia
mtindo wa peke yake katika sauti na mpangilio wa
mashairi anapotoa wimbo mpya. Huu ndio huitwa
mtindo. Katika fasihi andishi mtindo unaweza
kujitokeza kwa njia za kipekee za mtunzi katika
matumizi ya lugha, methali na misemo, msuko na
mpangilio wa vina na mizani katika ushairi.
c) Mandhari
Williady (2015) Mandhari ni eneo au mazingira ya
kweli au yakubuni ambayo hutumiwa na mwandishi
katika kuwajenga wahusika na uhusika wao.
d) Matumizi ya
Lugha
Williady (2015) Matumizi ya lugha ni ustadi wa
msanii katika kutumia lugha itakayoleta mvuto kwa
wasomaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi.
Katika kutumia lugha msanii lazima azingatie
kipengele cha uteuzi wa maneno yanayoendana na
hadhira yake, maneno hayo ndiyo yatakayoleta
mfungamanisho katika ya msanii, hadhira na
ujumbe uliokusudiwa.
e) Matumizi ya
tamathali za semi(usemi)
Williady (2015) Tamathali maanayake ni neon moja
au kifungu cha maneno kilicho sukwasukwa na
kufichwa maana.
Baadhi ya tamathali za semi katika Kiswahili ni
pamoja na;
Tashibiha, sitiari, tafsida, tashihisi, chuku,
kinaya,dhihaka, mbalagha,tabaini
f) Mbinu
nyingine za kisanaa
Hapa huwa na mchanganyiko wa mbinu kadhaa
katika usimulizi na silazima mbinu hizo zitumike
zote kwa wakati mmoja. Mfano wa mbinu hizo ni
pamoja na;
Takriri, kuchanganya ndimi, tanakali sauti, taswira,
lakabu, nahau na misemo
e) Wahusika
Williady (2015) wahusika ni viumbe hai au viumbe
ambao si hai wanaobebeshwa majukumu na
msanii ili kuwafikishia hadhira ujumbe
uliokusudiwa.
MAUDHUI KATIKA
FASIHI SIMULIZI
(williady: 2015) Maudhui ni jumla ya mawazo
anayoyazungumzia msanii au mtunzi katika kazi ya
fasihi.
Maudhui hujumuisha vipengele mbalimbali, kama
vile;Dhamira, ujumbe, falsafa, mafunzo, migogoro
na mtazamo.
TANBIHI: Kuna baadhi ya wataalamu wa lugha
wanakiweka kipengele cha migogoro upande wa
fani na kunabaadhi wanakiweka kipengele hiki
upande wa maudhui. Mimi nakiweka upande wa
maudhui kwa kuwa migogoro inabeba kwa kiasi
kikubwa ujumbe kuliko ufundi.
DHAMIRA
Dhamira ni shabaha kuu ya mtunzi wa kazi ya
fasihi. Shabaha hii ukusudiwa ni nani wakumlenga
nayo. Msanii anaweza kuwalenga kimaudhui
watoto, wanawake, wasomi au watu wote katika
jamii. Shabaha hii yaweza kuandikwa au
kutongolewa kwa mdomo ikiwa na lengo la
kupongeza, kuhimiza, kushauri, kutoa taarifa na
kukosoa.
UJUMBE
Ujumbe ni mawazo yanayotokana na dhamira,
mawazo haya yaweza kujitokeza waziwazi au kwa
kificho.
FALSAFA
Falsafa ni hekima hekima ya mtunzi. Mtunzi
huamini kuwa kupitia imani hii jamii inaweza
kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili. Kwa
mfano shekhe Shaaban Robert aliamini kuwa kila
mwanajamii akiwa na utu basi haki na upendo
vitapatikana kirahisi.
MAFUNZO
Mafunzo ni nasaha anazotoa mtunzi ambazo
huifundisha hadhira maadili Fulani. Maana ya
mafunzo hutegemea namna hadhira inavyofasili
nasaha hizo.
MIGOGORO
Migogoro ni misuguano au mikinzano ama
kutoelewana kati ya pande mbili au zaidi ndani ya
kazi za fasihi.
AINA ZA
MIGOGORO
Mgogoro kati ya mtu na
mtu
Mgogoro kati ya mtu na
jamii
Mgogoro kati ya jamii na
jamii
                                              Mgogoro wa nafsi
VI.
MTAZAMO
Mtazamo na jinsi mwandisi anavyotazama na
kuyachukulia matukio katika ulimwengu na athari
zake kwa wanajamii. Mfano waandishi wengi wa
mashairi wanamtazamoa huu “Kuibuka kwa maovu
mengi duniani kwasasa ni matokeo ya binadamu
kuasi dini.
Habari kwa hisani na mwalimu

Share: