Friday, May 6, 2016

TANZIA



Ulimwengu wa soka umepotelewa na mchezaji Patrick Ekeng raia wa Cameroon.
Patrick Ekeng,26 aliyekuwa akiicheza soka la kulipwa katika klabu ya Dinamo Bucharest nchini Romania alipatwa na umauti baada ya kuanguka uwanjani dakika ya 70 akiitumikia klabu yake hiyo.

Taarifa za kifo chake zilithibitishwa masaa mawili baada ya kufikishwa hospitali. Chama cha soka cha Cameroon kimeelezwa kusikitishwa na taarifa hzo kupitia ukurasa wake wa tweeter.

Patrick amekuwa mchezaji wa pili Mkameroon kufia uwanjani baada ya nguli MARC VIVIAN FOE kupoteza maisha akiichezea nchi yake dhidi ya Colombia kwenye mashindano ya mabingwa wa mabara nchini Ufaransa mwaka 2003.

R.I.P.Patrick.

Share: